""
Nimetanguliza hadithi hizo mbili kuonesha jinsi gani uislamu unapinga muislamu kumuua muislamu mwenzake.
KUJITOA MUHANGA NI NINI ??
Ni hali ya mtu mmoja kujiwekea mazingira yake kama mtego wa kuua kundi la watu kwa katika mazingira ya kujilipua akiwa amevaa mabomu au kipando chake kikiwa kimefungwa na mabomu.
Hali kama hii haijalishi kwenye kundi lengwa la watu (Target required) kuna muislamu,watoto,au wanawake ambao katika uislamu imekatazwa kuwadhulu endapo mpo katika viwanja vya vita.sasa iweje imani hii ya muhanga wa mabomu iwekwe katika uislamu ??
Utagundua kuna sababu zilizojificha za kujitolea muhanga ili kuuangamiza uislamu na lengo hasa la uislamu kwa vizazi changa vijavyo.
Maana halisi ya uislam ni salama na amani.
Hakuna hali yoyote ya kupigania uislamu kwa kujitoa uhai wako hali ya kuwa adui huyo wa uislamu yupo hai .kwa maana mabomu umejifunga wewe jee kama yatalipuka bila muhusika kufa utakuwa umeupigania uislamu ?? jibu moja kwa moja ni hapana.
Muislamu kumuua muislam mwenzake iwe kwa bahati mbaya ama kwa kukusudia imetengewa toba na Mwenyez MUNGU sub-hana hu wataala(Allah).kwa maana si ruhusa kwa hilo jambo,jee hatuoni kwenye muhanga waislam wanauawa ??
Tafakali na jifunze kwa hayo ALLAH AALAM
0 comments:
Post a Comment