Wednesday, September 6, 2017

YAJUE MATESO NA UNYONYAJI WANAOUPATA WAISLAM WA MYANMAR DHIDI YA SERIKALI NA BUDHA


Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Myanmar limetoa ripoti iliyofichua kuwa Waislamu katika maeneo yote ya nchi hiyo wanauawa na kuhujumiwa na wanajeshi wa nchi hiyo na sio wa kabila la Rohingya tu katika mkoa wa Rakhine.
Ripoti iliyotolewa jana Jumanne na Burma Human Rights Network imesema kuwa, serikali inawaunga mkono wanajeshi na mabudha wenye misimamo mikali kuwashambulia Waislamu katika kila pembe ya nchi hiyo ya mashariki mwa bara Asia.
Ripoti hiyo imesema kuwa, mbali na Waislamu wa Myanmar kunyimwa huduma za msingi kama matibabu wanapokwenda hospitalini, lakini pia serikali imekataa katakata kuwapa vitambulisho vya taifa.
Ripoti ya Burma Human Rights Network imebainisha kuwa, Waislamu katika miji na vijiji 46 nchini Myanmar wanapitia kila aina ya jinai kutoka kwa askari wa jeshi la nchi hiyo wakishirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali.
Mabudha wa Myanmar wanaoua Waislamu kwa msaada wa serikali
Tangu tarehe 25 Agosti mwaka huu, jeshi la Myanmar kwa kushirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali limekuwa likiwashambulia Waislamu wa jimbo la Rakhine, ambapo zaidi ya 400 miongoni mwao wamekwishauawa, huku wengine zaidi ya laki 1 na 25 elfu wakikimbilia Bagladesh.
Mauaji na jinai hizi zinafanyika mkabala wa kimya cha taasisi husika za kimataifa kama vile Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya kikosi cha ulinzi wa mpakani cha Bangladesh, kwa akali watoto 11 na wanawake 15 Waislamu wa Myanmar wamefariki dunia katika tukio hilo. Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, zaidi ya nyumba 2600 za Waislamu wa jamii ya Rohingya katika jimbo la Rakhine lililoko magharibi mwa Myanmar zimechomwa moto na jeshi la nchi hiyo.
Ripoti ya Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) inaonyesha kuwa, takribani Waislamu elfu sitini wa Kirohingya wamekimbilia nchini Bangladesh baada ya kushadidi mauaji na vitendo vya ukandamizaji dhidi yao. Duru mpya ya vitendo vya utumiaji mabavu na mauaji dhidi ya Waislamu wa Kirohingya ilianza baada ya jeshi la Myanmar kupeleka kikosi katika jimbo la Rakhine la magharibi mwa nchi hiyo.
Waislamu wa Myanmar wakiyahama makazi yao
Licha ya malalamiko ya duru za kisiasa kuhusiana na matokeo mabaya ya kutumwa jeshi huko Rakhine, lakini serikali ya Myanmar ilidai kuwa, kikosi hicho kimetumwa huko ili kudhamini usalama na kuwalinda Waislamu hao. Hii ni katika hali ambayo, ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa, wanajeshi wa Myanmar wamekuwa wakihusika moja kwa moja na mauaji dhidi ya Waislamu hao.
Ripoti mbalimbali za kuaminika zinaonyesha kuwa, baadhi ya Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakiuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi hao au kupitia hujuma ya mabudha wenye misimamo ya kufurutu ada ambao nao wamekuwa wakipata himaya ya jeshi.
Aidha Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakipoteza maisha kwa kuzama boti wanazosafiria wakikimbia hujuma za mabudha na wengine hufa kwa njaa wakiwa njiani huku baadhi yao wakitangatanga katika misitu na baharini wakiwa katika juhudi za kukimbia vitendo vya utumiaji mabavu vinavyowalenga. 
Wanajeshi wa Myanmar wanaotuhumiwa kuwaua Waislamu wa Rohingya
Hii ni katika hali ambayo, baada ya kufanyika marekebisho ya kisiasa na kiuchumi nchini Myanmar walimwengu walikuwa wakitaraji kwamba, serikali ya nchi hiyo itachukua hatua ya kulipatia ufumbuzi tatizio la Waislamu wa Rohingya.
Kwani kimsingi hatua ya serikali ya Myanmar ya kuwanyima haki ya uraia Waislamu hao ndio iliyoandaa uwanja wa mauaji na vitendo vya kinyama dhidi yao.
Marie Lall, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Heidelberg  cha nchini Ujerumani na mtaalamu wa masuala ya Myanmar anasema: Baada ya kufanyika marekebisho ya kiuchumi na kisiasa nchini Myanmar, licha ya kuwa hali ya kifedha ya watu katika miji imeboreka, lakini faida ya hilo sio tu kwamba, na haiyafikii maeneo ya vijijini na viunga vyake, bali hali hii imezidisha mazingira magumu kwa akthari ya jamii za waliowachache kuweza kumiliki nyumba na makazi.
Mabudha wenye misimamo mikali wa Myanmar ambao wamekuwa wakiwahujumu na kuwaua Waislamu wa Kirohingya
Ramzy Baroud mwandishi wa habari Mmarekani mwenye asili ya Palestina ambaye anaishi Washington anasema: Baada ya Myanmar kuondolewa vikwazo, ulimwengu wa Magharibi ulipata fursa mwafaka ya kunufaika na vyanzo vya utajiri vya nchi hiyo na hili ni jambo ambalo linapewa kipaumbe na madola ya Magharibi kuliko hata suala la haki za binadamu. Ni kwa mintarafu hiyo ndio maana madola hayo yamenyamazia kimya mauaji dhidi ya Waislamu wa Myanmar na yanachokifuatilia katika nchi hiyo ni maslahi yao ya kiuchumi tu.
Vyovyote itakavyokuwa, inavyoonekana ni kuwa, nchi na asasi za Kiislamu ndizo zinazoweza kuchukua hatua za maana za kuhitimisha jinai za jeshi la Myanmar na mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Walislamu wa Rohingya. Indonesia na Malaysia zikiwa nchi za Kiislamu wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini na Mashariki mwa Asia ambapo Myanmar pia ni mwanachama katika jumuiya hiyo, zina jukumu zito zaidi la kuzuia unyama na ukatili dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya.
Huku utawala wa mabudha wa Myanmar ukiendeleza ukatili wake dhidi ya Waislamu wa Rohingya, utawala wa Kizayuni wa Israel unaowakandamiza kikatili Waislamu wa Palestina nao unaimarisha ushirikiano wake wa kijeshi na serikali ya Myanmar.
Gazeti la Haaretz la utawala wa Kizayuni limeripoti leo (Jumatatu) kuwa katika ziara ya mwaka jana ya nchini Myanmar ya Michel Ben-Baruch, mkuu wa kitengo cha utawala wa Kizayuni cha kusafirisha nje vifaa vya kijeshi, utawala wa Kizayuni ulikubaliana na nchi hiyo kuiuzia boti za kisasa za kivita.
Wahanga wakuu wa ukatili wa mabudha wa Myanmar wanaoungwa mkono na Israel ni watoto na wanawake Waislamu

Wakati huo huo afisa mmoja wa baraza la kijeshi la Myanmar mwaka 2015 alitembelea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kuonana na mkuu wa jeshi wa Israel.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, Waislamu 90 elfu wamekimbia makazi yao katika jimbo la Rakhine katika kipindi cha siku 10 zilizopita kutokana na ukatili mkubwa wanaofanyiwa na wanajeshi wa serikali ya Kibudha ya Myanmar.
Serikali ya nchi hiyo inawanyima Waislamu karibu milioni moja wa Rohingya hata haki zao za kimsingi kabisa kama vile uraia. 
Hadi hivi sasa maelfu ya Waislamu wa Rohingya wameshauawa na makumi ya maelfu  ya wengine wamelazimika kuyakimbia makazi yao.

0 comments:

Post a Comment

MWEZI WA MUHARRAAM NA UZUSHI

بسم الله الرحمن الرحيم MASHIA NA BIDAA ZA MWEZI WA MUHARRAMU. Mwezi wa Muharramu ni miongoni mwa miezi mitukufu kwa mujibu wa mafundis...