Friday, September 29, 2017

MWEZI WA MUHARRAAM NA UZUSHI

بسم الله الرحمن الرحيم

MASHIA NA BIDAA ZA MWEZI WA MUHARRAMU.

Mwezi wa Muharramu ni miongoni mwa miezi mitukufu kwa mujibu wa mafundisho ya  kiislamu.

Mwezi huu tumefudishwa kufunga swaumu ya Ashuuraa na kufanya  kheri nyinginezo kwa kutaraji malipo.

Mwezi huu una kumbukumbu kwa Waislamu kwa  tukio kubwa la kuhama Mtume wa Allah Swalla llaahu alayhi wasalama kutoka Makkah kuhamia Madinah.

Allah mtukufu pia akajaalia kifo cha Husein lbnu Aliy Radhia llaahu  anhu mjukuu wa Mtume swalla llaahu alayhi wasallama kutokea mwezi huu  huko Karbala nchini lraqi kwa kuuwawa kwa dhulma.

Mashia wakachukua tukio la kifo cha Husein  Radhia llaahu anhu ndani ya mwezi huu kufanya maadhimisho yaliyo jaa Bidaa na Munkari na kuziacha Sunna zenye fadhila ndani yake, wakajibidisha kutekeleza Bidaa wanazo amini ni kukienzi kizazi cha Mtume Swalla llaahu alayhi waalihi wasallama.

Mashia weameacha Sunna ya kufunga  mwezi huu (Ashuuraa) huku wakiwatuhumu wote wanaofunga wanafunga kwa kuunga mkono na kusherehekea kuuwawa Husein lbnu Aliy Radhia llaahu anhu.

Mashia wapo baadhi yao hawali nyama mwezi huu wa Muharram hususan siku ya mwezi kumi,siku ambayo ameuliwa Husein lbnu Aliy Radhia llahu anhu,kwa kudai siyo vizuri siku ambayo damu ya mjukuu wa Mtume swalla llaahu alayhi wasallama imemwagika halafu wao wale nyama.

Wakristo nao baadhi yao hawali nyama siku ya ljumaa kuu ya Pasaka,siku ambayo wanadai Yesu aliteswa na kuuwawa Msalabani,hivyo haiwezekani kula nyama siku ambayo kiongozi wao amemwaga damu Msalabani.

Wapo Mashia ambao hawawezi kufunga ndoa mwezi huu kwa kudai ndoa ni jambo lenye furaha ,nao wako ndani ya huzuni hawawezi kufanya jambo la furaha, ni sawa na kupuuza kifo cha Husein Ibnu Aliy.

Mwezi huu ni mwezi wa kuimba nyimbo za kuomboleza msiba na kulaani waliomuua Husein na wengine wote wanaopinga maadhimisho yao huku wakiwatuhumu kufurahia au kutojali mauaji hayo.

lmekuja katika kitabu مفاتيح الجنان mlango unaozungumzia matendo ya mwezi wa Muharram.

 وينبغي للشيعة أن يمسكوا عن السعي في الحوائج دنياهم وأن لايدخروا فيه شيأ لمنازلهم وأن يتفرغوا فيه للبكاء والنياح وذكر المصائب،وأن يقيموا مآتم الحسين  عليه السلام، وأن يجتهدوافي سب قاتليه ولعنهم ،والأ حسن لايصام اليوم التا سع والعاشر فإن بني أمية كانت تصومها شماتة بالحسين عليه السلام وتبركا بقتله،وقد افترواعلى رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم أحاديث كثيرة وضعوها في فضل هاذين يومين وفضل صيامهما( مفاتيح الجنان،فصل في أعمال شهر محرم،ص352-353،دار القربى للطباعة والنشر)

lnatakiwa Mashia wajizuilie kutembea kwa ajili ya mambo ya dunia yao siku hiyo ya Ashura,na wasilimbikize chochote majumbani mwao,na wakae faragha kwa ajili ya kulia na kuomboleza na kutaja matukio (kuhusu Husein) na wajipige kifuani kwa ajili ya Husein   amani juu yake,pia wajitahidi kuwatukana waliomuua na kuwalaani,na wapeane pole wenyewe kwa wenyewe(Taazia).Na lililo bora wasifunge siku ya tisa na kumi (Mwezi Muharram) hakika banu Umayyah walikua wanafunga masiku hayo kufurahia kifo cha Husein alayhi ssalaam na kutaka baraka kwa kifo chake.Hakika (hao banu Umayyah)wamezusha hadithi nyingi juu ya Mtume swalla llaahu alayhi wasallama wakaweka katika fadhila za masiku haya mawili (9 - 10) na fadhila ya swaumu yake.
(Mafaatiyhul Jinaan,mlango,Matendo ya mwezi wa Muharramu,Uk 352-353,chapa ya Daarul Qurbaa).

Je Mashia wanafunga mwezi Muharram kama wafungavyo Waislamu wengine?.

وينبغي أيضا للشيعة الإمساك عن الطعام والشراب في هاذا اليوم من دون نية الصيام وأن يفطروا في آخر النهار بعد العصر بما يقتات به أهل المصا ئب كاللبن الخا ثر والحليب.  ونظا ئر هما لا با لأغذية اللذيذة.

 Na yatakikana pia kwa Mashia kujizuilia  kula na kunywa  siku hii pasi na kunuia kufunga na wafuturu mwishoni mwa mchana baada ya Al asri kwa kile  walichokula watu wa masaibu (ya Karbala) kama maziwa na maziwa  ya mgando na muonekano wake  isiwe chakula kitamu.(Rejea ni hiyo hiyo hapo juu).

Wakristo nao hufunga msimu wa Pasaka siku 40 mfululizo,kuanzia mwezi wa tatu wote (March)hadi  masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa nne (April),mwezi wa nne ndiyo mwezi wa Pasaka, hujizuia kula na kunywa ,funga hii wanafungua sa 12 jioni ,na wenye matatizo kama maradhi wanaweza kufungua saa 9 au 10, lengo la kufunga ni kushinda na njaa kama alivyo  shindaYesu kwa siku arobaini.Mashia nao wanashinda na njaa hadi jioni (Al asri) kama walivyo shinda watu wa tukio la mauaji ya Husein Karbalaa.

Ukimuuliza Shia juu ya Bidaa wazifanyazo mwezi wa Muharramu uhalali wake katika dini atakushutumu hukipendi kizazi cha Mtume swalla llaahu alayhi wasallama,au utaishia kuambiwa wewe ni Wahabi tu,una chuki na Ahlul Bayti,au umebahatika utajibiwa hayo yanayo fanywa ya kujipiga kijitoa damu,kutembea juu ya moto ,kubeba  majeneza na mikuki huo ni ujinga wao tu hao wafanyao,kwani hayamo katika Ushia.

Ni kweli hayamo katika  Ushia? Wenyewe watatufahamisha kupitia vitabu vyao.

(a)KUCHANA NGUO KWA AJILI. YA MSIBA.

عن حيان بن سديرقال،سألت أبا عبد الله عليه السلام عن الرجل   شق ثوبه على أخيه أو على  أخته أو على قريب له؟فقال لابأس بشق الجيوب   فقد شق موسى  بن عمران عليه السلام جيبه على أخيه هارون(تهذيب الإحكام،8/325،وسائل الشيعة22/304)

Amesimulia Hayyaan lbnu Sadiyr(au Sudayr) amesema,Nilimuuliza Abu Abdillaahi alayhi ssalaam juu ya mtu aliye chana nguo juu msiba wa nduguye,au dada yake,au mtu wa karibu yake?akasema hapana shaka (kwa ajili ya msiba)ni sawa kuchana nguo.  Hakika amechana Musa lbnu lmraan nguo yake juu ya kifo cha nduguye  Haarun.(Tahdhiybul Ahkaam 8/325,Wasaailu Shiiah 22/304).

(b)KUJIPIGA MAKOFI.

Amesema mwandishi wa kitabu Ashaairul Husayniyah,Sheikh Muhamad Jumaa Baadiy.

ومن حق هؤلاء الذين لم يعرفوا الحسين عليه السلام ولم يشربوا كأس محبته ولم يحزنوا في مصيبته أن يتعجبوا من مظا هر الشيعة في أحزانهم عليه ،فإن حبهم المتجذر في النفوس دفعهم إلى لطم الصدور ووجوه والرؤوس في المآتم.(الشعائر الحسينية،ص134، اللطم).

Kutokana na ukweli wa hawa ambao hawamjui Husein alayhi ssalaam,na hawaja kunywa  kikombe cha mapenzi yake,na hawahuzuniki kwa msiba wake wanastaajabia muonekano wa Mashia katika kumuhuzunkia huyo (Husein) Hakika mapenzi yao ni yenye kuchipua kutoka nafsini mwao,yakawasukuma kupiga vifua na nyuso na vichwa katika maombolezo.(Ashaairul Husayniyyah Ukr 134).

Wanasema Mashia hata Malaika  (Mahurlul ayni) Peponi hujipiga makofi kwa ajili ya Husein,kwa maana inayopatikana katika ziara ya Swaahibul Aswri alayhi ssalaam (Imam Mahdi),pale alipo mzuru babu yake Husein alayhi ssalaam  alisema.

"وأقيمت لك المأتم في أعلى عليين،ولطمت عليك حور العين"(بحار الأنوار 97/322).

Na wamefanya(Malaika) maombolezo kwa ajili yako juu mbingu ya saba,Na wamejipiga makofi kwa ajili yako(Mahuuril ayni) Malaika wa peponi.(Bihaarul Anwaar 97/322)

(c)KUJIKATA MIILI YAO HADI KUTOA DAMU.

Amesema mwandishi  Mshia wa kitabu Ashaairul Husayniyyah ukurasa wa 138.

وظاهر فتاوى كثير من العلماء الإعتماد على هذا الخبر المرسل في جواز الإدماء،وأفتى عامة الفقهاء برجحا نه واستحبابه لكونه أجلى مصاديق الجزع علئ الإمام الحسين عليه السلام عملا بهذه الرواية.

Na dhahiri fatawa za wengi miongoni mwa Maulamaa ni (kwamba).wanaitegemea habari hii ambayo ni mursal (juu ya kujipiga na) kujitoa damu,na wanachuoni wote wa fiqhi wametoa fatwa kwa kulipa nguvu (hilo) na kulipendekeza kwa kuwa ni jambo kubwa zaidi lenye kujulisha kumuhuzunikia Husein alayhi ssalaam kwa ajili ya kuifanyia kazi riwaya hii.

Anachosema ni kwamba wanachuoni wa kishia wameitegemea riwaya Mursal (Hadithi dhaifu) kutoa fatwa kujuzisha kujipiga na kujitoa damu,ila huko kujipiga na kujitoa damu wanafanya kwa sababu kunaonyesha kumuhuzunikia lmam Husein.

Akaeleza tena juu ya hilohilo la kujitoa damu.

قال الشيخ محمد حسين النا ئيني ،لاإشكال في جواز اللطم بالأيدي على الخدود والصدور إلى حد الإحمرار والإسوداد،بل يقوى جواز الضرب با لسلاسل أيضا على الأكتاف والظهور إلى حد المذكور ،بل وإن تأدى كل من اللطم والضرب  إلى خروج دم يسير على الأقوى،وأما إخراج الدم من النا صية با لسيوف والقامات فالأقوا جواز ما كان ضرره مأمونا ،وكان  من مجرد  إخراج الدم من النا صية بلا صدمةعلى عظمها،ولا يتعقب عادة بخروج ما يضر خروجه من الدم ونحوذلك كما يعرفه المتدبرون العارفون بكيفية الضرب ولوكان عند الضرب مأمون ضرره بحسب العادة،ولكن إتفق خروج قدر ما يضر خروجه لم يكن ذلك موجبالحرمته،ويكون كمن توضأ أو اغتسل أو صام أمنا من ضرره ثم تبين ضرره منه (الشعائر الحسينية ص 144،وفتاوى الشعائر الحسينية،ص21)

Amesema Sheikh Muhamad  Husein Annaaiyniy,Hakuna shaka juu ya kufaa kujipiga kwa mikono mashavuni na kifuani mpaka kujitia wekendu na weusi,bali inapata nguvu kauli ya kufaa kujipiga kwa minyororo juu ya mabega na mgongoni mpaka kufikia hivyo ilivyo tajwa(wekundu na weusi),Bali hakuna ubaya hata kama itapelekea kutoka damu kidogo kwa kauli yenye nguvu,Ama kujitoa damu utosini kwa Upanga na ncha zake,kwa kauli yenye nguvu inajuzu kiasi cha kuwa madhara yake siyo makubwa kwa kiasi cha kujitoa damu kwenye utosi pasi na kuugonga mfupa wake na isifuate kutoka kile ambacho kina madhara(iwe ubongo) ,kama wanavyo jua hilo wenye wenye uzoefu kuhusu namna ya kujipiga na hata kama wakati wa kujipiga anakua ni mwenye kujiaminisha na madhara,LAKINI AKITOA DAMU KIASI CHENYE KUJIDHURU BASI HILO SIYO HARAMU,ni sawa na mtu aliye tawadha ,kuoga au kufunga akiwa na amani kwamba hatodhurika kisha akapata madhara.(Ashaairul Husayniyah Ukr 144,Fataawa,Shaairul Husayniyah Ukr 21).

Kama kawaida ya Mashia,jambo lao hawakosi kulijaza fadhila nyingi ili liendelee kudumishwa hata kama liko kinyume kabisa na mafundisho ya Uislamu,zifuatazo ni Riwaya zao juu ya fadhila za kuzuru kaburi la Husein Radhia llahu anhu huko Karbalaa nchini lraqi.

عن بشير الدهان قال،سمعت أبا عبد الله عليه السلام ،من زارقبر الحسين عليه السلام  يوم عرفة،فكأنما زار الله تبارك وتعالى في عرشه. (بحار الأنوار 87/97)

Amesimulia Bashir Adahhaan amesema,Nimemsikia Abuu Abdillaahi alayhi ssalaam,Mwenye kuzuru kaburi la Husein alayhi ssalaam siku ya Arafa,kana kwamba amemzuru Allah mtukufu katika Arshi yake.(Bihaarul Anwaar 87/89)

عن داود بن كثير،عن أبي عبد الله عليه السلام قال، إن فاطمة بنت محمد عليها السلام تحضرلزواز قبر ابنها الحسين عليه السلام فتستغفر لهم ذنوبهم(كامل الزيارات)

Amesimulia Daud lbnu Kathir,kutoka kwa Abuu Kaa alayhi ssalaam amesema, Hakika Fatma bint Muhammad alayha ssalaam,anahudhuria kwa wanaolizuru kaburi la mtoto wake Husein amani juu yake na  anwaombea msamaha madhambi yao.(Kaamilu Ziyaaraati)

عن إسحاق بن عمار قال،سمعت أبا عبد الله عليه السلام يقول،ليس النبي في السماوات والأرض إلا يسألون الله تعالى أن يأذن لهم في زيارة الحسين عليه السلام،ففوج ينزل وفوج يصعد(كامل الزيارات-البحار101)

Amesimulia Ishaqa lbnu Ammar amesema,Nimemsikia baba Abdillahi alayhi ssalaam anasema,Hakuna Nabii mbinguni na ardhini ila anamuomba Allah mtukufu amruhusu   (ahudhurie) katika kumzuru Husein alayhi ssalaam,makundi wanateremka na makundi wanapanda.(Kaamilu Ziyaaraati -Albihaaru 101)

عن يونس،عن أبي عبد الله عليه السلام قال،من زار قبر الحسين عليه السلام يوم عرفة،كتب الله أالفاألفا حجة مع القائم،وإلفا ألفا عمرة مع رسول الله صلى الله عليه وسلم(كامل الزيارات ص172)

Amesimulia Yunus,kutoka kwa Abuu Abdillahi alayhi ssalaam amesema,Mwenye kuzuru kaburi la Husein alayhi ssalaam siku ya Arafa,humuandikia Allah maelfu kwa maelfu ya hija pamoja na lmam Mahdi,na maelfu kwa maelfu ya Umra pamoja na Mtume swalla llaahu alayhi wasallama(Kaamilu Ziyaaraati,Ikr 172)

عن أبي عبد الله عليه السلام قال،طين قبر الحسين الشفاء من كل داء وهو الدواء الأكبر(البحار 101)

Amesimulia Abu Abdillahi alayhi ssalaam  amesema,Udongo wa kaburi la Husein ni dawa ya kila ugonjwa,nao ni dawa kubwa(Albihaaru 101)

قال الصادق عليه السلام،السجود على طين الحسين ينور إلى أرض السابعة(الفقيه ج-1)

Amesema Aswaadiqu alayhi ssalaam,Kusujudu juu ya udongo wa (Kaburi la Husein) kunatoa nuru mpaka ardhi ya saba (Alfaqiyhu- jz-1)

عن أبي عبد الله عليه السلام قال، من أتى الحسين عارفا بحقه كتب الله في أعلى عليين(البحار 101)

Amesimulia Abuu Abdillahi alayhi ssalaam amesema,Mwenye kumuendea Husein huku akijua haki yake humuandika Allah juu mbingu ya saba(Albihaaru 101)

عن  علي بن أسبط ،عن أبي عبد الله علبه السلام ،قا ل إن زيارة قبر الحسين عليه السلام أفضل من حج بيت الله الحرام،بل إن  زوار الحسين أطهار،وأهل الموقف فيهم إبناء زنا(بحار الأنوار 87/98)

Amesimulia Aliy lbnu Asbaatwi,  kutoka kwa Abuu Abillaahi alayhi ssalaam amesema,Hakika kuzuru kaburi la Husein alayhi ssalaam ni bora kuliko kuhiji nyumba ya Allah tukufu (Alkaaba) Lakini hakika wanaomzuru Husein wametwaharika,na watu wa Arafa katika wao kuna watoto wa Zinaa(Bihaarul Anwaaru 87/98)

عن أبي عبد الله عليه السلام قال،إن الله تبارك وتعالى ليبدأ بأهل قبر الحسين  عليه السلام قبل أهل العرفات(بحار الأنوار 87/98)
.
Amesimulia Abuu Abdillahi alayhi ssalaam amesema,Hakika Allah mtukufu huanza (kuwatazama) watu waliopo kaburi la Husein alayhi ssalaam,kabla ya watu waliopo Arafah (Bihaarul Anwaar 87/98).

Kwa mujibu wa fadhila hizi za kuzuru kaburi la Husein Radhia llaahu anhu huko Karbala lraqi basi Mashia kwao Hija haina thamani mbele ya kuzuru kaburi la Husein Radhia llaahu anhu.

Jambo la Husein limeleta mtihani kwa Mashia kama ifuatavyo.

(1)Wapo wanao huzunika tu,
(2)Wengine hudondosha machozi.
(3)Wengine hulia kwa kwikwi.
(4)Wengine hupiga mayowe.
(5)Wapo wanaojipiga kifuani.
(6)Wengine hujipiga makofi.
(7)Wengine hujipiga utosini.
(8)Wengine huchana nguo zao.
(9)Wengine hujipiga minyororo     mabegani.
(10)Wengine hujipiga visu migongoni.
(11)Wengine hijikata upanga utosini au mgongoni.
(12)Wengine huchomwa sindano utosini na kutolewa damu.
(13) Wengine hubeba majeneza na mikuki.
(14)Wapo wanao jitaabisha kwa kuswali au kutembea juu ya moto.
(15)Wapo wanao tambaa kwa tumbo kuliendea kaburi la  Husein huko Karbalaa
(16)Wapo wanao muadhibu mnyama kwa niaba ya mtu ambae wanaamini alikua ni adui wa Ahlul Bayti kama Yazidi lbnu Muawiyah na wengineo wanao watuhumu ubaya dhidi ya Ahlul Bayti.

Yote haya hufanyika kwa madai ya kumpenda Husein na huzuni juu yake,ukipinga unahukumiwa kuwachukia Ahlul Bayti.

La kushangaza,wameuliwa Manabii alayhimu Ssalaam kwa dhulma lakini wafuasi wao hawakufanya haya,wameuliwa Maswahaba kama Hamza na wengine Allah awaridhie,lakini Mtume swalla llaahu alayhi wasallama hakufanya haya wafanyayo Mashia.

Amekufa Mtume swalla llaahu alayhi wasallama, na Mashia wanasema ameuliwa na wake zake wawili Aisha na Hafsa  Allah awaridhie kwa kumnywesha Sumu nacho ni kifo cha dhulma, Mtume pia alikuwa mtetezi wa haki kwa Ulimwengu wote,mbona Ahlul Bayti hawakufanya hayo?,na mbona Mashia hawaombolezi kifo cha Mtume kwa vishindo nao wanadai ameuliwa kwa dhulma?,Au Mtume hakua mtetezi wa haki za watu wote kama Husein?.

(Kuuhusu  Mtume kuuliwa na wake zake,Tazama tafsiri ya Mayunga chapa ya pili ukrasa wa 187 na Alburhan fiy tafsiri lqur-an ya  Sayyid Haashimul Bahraaniy katika ufafanuzi wa Surati Ttahriym aya ya 1 -2. kifungu cha 5,hao wote ni Mashia).

Mashia mila hii wameitoa wapi?

Mila hii ya kutomaliza  kuomboleza msiba waanzilishi ni Wakristo,kama waombolezavyo kifo cha nabii  lsa alayhi ssalaam kila mwaka kwa vilio ,matembezi na kujipiga au kumtungika mmoja wao Msalabani wakamsulubu pengine hadi kifo hasa sehemu za Amerka ya kusini.Mashia nao husimama Sayyid wao na upanga mkononi akiwachanja utosini wafuasi wake wakiwemo na watoto wadogo wasiojua maaa ya jambo hilo,nako ni kuwasulubu pia hakika mwili hauchezewi kiurahisi sampuli hiyo.

Mashia wa huku kwetu kuna mambo hawajafikia kuyafanya kwa sababu imani zao hazijakomaa kama Mashia wa huko Asia,wasitudanganye kwamba hayamo katika Ushia ,ukweli yameruhusiwa tena ni kiwango cha juu cha mapenzi ya Husein  Radhia llaahu anhu.

TANBIHI.

Waliofia Karbala wameuliwa hawakujiua,wewe ukijiua kwa kujipiga au kujitoa damu umejiua mwenyewe,Amesema Allah mtukufu.

قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُمْ بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا

Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo vyao?(Alkahfi 103)

الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا

Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri.(Alkahfi 104)

Tunamuomba Allah atuonyeshe haki na tuweze kuifuata.

والله أعلم.

Thursday, September 21, 2017

KISA CHENYE MAZINGATIOO

Kisa enzi za Nabii Musa

Wakati mmoja enzi za nabii mussa a.s ilikuwepo familia moja ya watu wawili yaani mume pmj na mke wake.

Familia hiyo ilikuwa ni familia duni sana hawakuweza kumudu ata chakula chao cha kila siku.

Waliishi ktk hali hiyo ya ufukara na umaskini uliopitiliza tokea wafunge ndoa wakivumiliana kwa hali hiyo waliyokuwa nayo.

Siku moja walipokuwa pmj kitandani mke akasema kumwambia mume wake.

"Mume wng hivi mussa a.s si ni nabii wa m/mungu tena anaongea nae.?"

Mume akamjibu mke wake kuwa ndivyo.

Mke akamwambia "ni kwa nn tusiende kwa nabii musaa a.s tumueleze juu ya hali yetu na ufukara tuliokuwa nao,

Kisha tumtake akatufikishie habari zetu hizi kwa m/mungu na atuombee ili nasi walau tuweze kumiliki chochote (kipato) ktk maisha yetu yaliyobakia!"

Mume akamuafiki mke wake kwa kumuambia kuwa ni mawazo mazuri.

Basi asubuhi kulipo pambazuka mume akatoka na kuelekea kwa nabii mussa a.s na kumuelezea juu ya hali yao

Na akimtaka akamfikishie habari hiyo kwa m/mungu na awaombee ili hali yao ibadilike walau nao waweze kuwa miongoni mwa waliokuwa navyo.

Nabii musaa a.s akatoka kwenda kuongea na mola wake juu ya hali ya familia ile.

M/mungu akamwambia nabii mussa a.s "ewe mussa a.s waambie kuwa nitawakunjulia rizki watakuwa na maisha mazuri,,,,,

Lakini kwa muda wa mwaka mmoja tu peke yake mwaka huo ukiisha watarudi tena ktk hali yao ya awali ya ufukara."

Nabii mussa a.s akarudi na kuwajulisha kuwa m/mungu amewakubalia maombi yao lkn atawaneemesha kwa muda wa mwaka mmoja tu.

Wale wanandoa wakazipokea taarifa hizo na baada ya muda mambo yakaanza kubadilika .

Ikawa wanapata kipato kwa njia ambayo wasiyoijua wala kutarajia.

Maisha yakaanza kubadilika na wakawa ni miongoni mwa watu waliokuwa navyo (matajiri).

Mke akasema kumwambia mume wake "mume wng hivi unakumbuka kuwa hali hii tuliyokuwa nayo na mali hizi ni kwa muda wa mwaka mmoja tu,,,,

Mwaka ukiisha tutarudi tena ktk hali yetu ile ile ya ufukara tuliyokuwa nayo?"

Mume akamuitikia kuwa ndio anakumbuka.

Mke akamwambia "kwa ajili hiyo ww unalionaje hili,,,,tunajenga umaarufu kwa pesa tuliyokuwa nayo na tunafanya starehe.

Mpaka watu wote wakajua juu ya utajiri wetu lkn mwaka ukiisha watu watakuwa wakisema kuwa tulikuwa matajiri lkn sasa ata ela ya kula hawana!"

Mume akamwambia mke wake "umenishauri jambo zuri ewe mke wng ni lazima tufanya jambo."

Wakaanza kujenga nymba sehemu za pembezoni mwa mabarabara za wasafiri.

Nyumba hizo wakizigawanya ktk sehemu saba tofauti tofauti.

Ktk nyumba hizo wakawaajiri watu wakiwahudumia wasafiri wanaopita sehemu hiyo kwa vyakula na vinywaji pasina malipo yoyote.

Wakawa wakishughulika na jambo hilo wakiwalisha wasafiri wapitao hapo usiku na mchana.

Siku miezi iliisha nabii mussa a.s akiwatazama juu ya hali waliyokuwa nayo pmj na utajiri wao.

Mwaka uliisha wakiwa ktk hali yao ile ile ya utajiri huku  wakiendelea kuwahudumia watu.

Na hatimae ukaingia mwaka mwingine tena ilihali hali ya wale wanandoa ikiwa vile vile ya utajiri.

Nabii mussa a.s akashangaa na kwenda kumuuliza allah s,w

Nabii mussa akasema "ewe mola wangu ulisema kuwa utawapa mali kwa muda wa mwaka mmoja, na mwaka ukiisha watarudi ktk hali yao ya ufukara,

Ni kwa nn sasa mwaka umeisha na umeingia mwaka mwingine ilihali wale watu wakiwa ktk hali yao ile ile ya utajiri?"

M/mungu s,w akamjibu nabii mussa a.s akamwambia

 "ewe mussa a.s mimi niliwafungulia mlango wng miongoni mwa milango yng ya rizki,

Wao wakafungua milango saba wakiwahudumia waja wng,

Ewe mussa a,s (kwa hilo walifanyalo) hivi ww ata huwaonei haya,

Ewe nabii mussa a.s hivi kiumbe anaweza kuwa ni mkarimu kunishinda mm mola wake.",,,,,,,,,,,,,,,,,,

Kuna msemo nausikia sana wakisema kuwa

" hakuna tajiri (aliyekuwa nacho) aliyewahi kufirisika kwa sababu ya kuwasaidia wengine. "

Mali inayotolewa kwa ajili ya kuwasaidia wengine m/mungu huizidisha mali hiyo kwa mtoaji.

Wednesday, September 6, 2017

YAJUE MATESO NA UNYONYAJI WANAOUPATA WAISLAM WA MYANMAR DHIDI YA SERIKALI NA BUDHA


Shirika moja la kutetea haki za binadamu nchini Myanmar limetoa ripoti iliyofichua kuwa Waislamu katika maeneo yote ya nchi hiyo wanauawa na kuhujumiwa na wanajeshi wa nchi hiyo na sio wa kabila la Rohingya tu katika mkoa wa Rakhine.
Ripoti iliyotolewa jana Jumanne na Burma Human Rights Network imesema kuwa, serikali inawaunga mkono wanajeshi na mabudha wenye misimamo mikali kuwashambulia Waislamu katika kila pembe ya nchi hiyo ya mashariki mwa bara Asia.
Ripoti hiyo imesema kuwa, mbali na Waislamu wa Myanmar kunyimwa huduma za msingi kama matibabu wanapokwenda hospitalini, lakini pia serikali imekataa katakata kuwapa vitambulisho vya taifa.
Ripoti ya Burma Human Rights Network imebainisha kuwa, Waislamu katika miji na vijiji 46 nchini Myanmar wanapitia kila aina ya jinai kutoka kwa askari wa jeshi la nchi hiyo wakishirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali.
Mabudha wa Myanmar wanaoua Waislamu kwa msaada wa serikali
Tangu tarehe 25 Agosti mwaka huu, jeshi la Myanmar kwa kushirikiana na Mabudha wenye misimamo mikali limekuwa likiwashambulia Waislamu wa jimbo la Rakhine, ambapo zaidi ya 400 miongoni mwao wamekwishauawa, huku wengine zaidi ya laki 1 na 25 elfu wakikimbilia Bagladesh.
Mauaji na jinai hizi zinafanyika mkabala wa kimya cha taasisi husika za kimataifa kama vile Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. 

Kwa mujibu wa taarifa rasmi ya kikosi cha ulinzi wa mpakani cha Bangladesh, kwa akali watoto 11 na wanawake 15 Waislamu wa Myanmar wamefariki dunia katika tukio hilo. Wakati huo huo, Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, zaidi ya nyumba 2600 za Waislamu wa jamii ya Rohingya katika jimbo la Rakhine lililoko magharibi mwa Myanmar zimechomwa moto na jeshi la nchi hiyo.
Ripoti ya Shirika la Kuhudumia Wakimbizi la Umoja wa Mataifa (UNHCR) inaonyesha kuwa, takribani Waislamu elfu sitini wa Kirohingya wamekimbilia nchini Bangladesh baada ya kushadidi mauaji na vitendo vya ukandamizaji dhidi yao. Duru mpya ya vitendo vya utumiaji mabavu na mauaji dhidi ya Waislamu wa Kirohingya ilianza baada ya jeshi la Myanmar kupeleka kikosi katika jimbo la Rakhine la magharibi mwa nchi hiyo.
Waislamu wa Myanmar wakiyahama makazi yao
Licha ya malalamiko ya duru za kisiasa kuhusiana na matokeo mabaya ya kutumwa jeshi huko Rakhine, lakini serikali ya Myanmar ilidai kuwa, kikosi hicho kimetumwa huko ili kudhamini usalama na kuwalinda Waislamu hao. Hii ni katika hali ambayo, ripoti mbalimbali zinaonyesha kuwa, wanajeshi wa Myanmar wamekuwa wakihusika moja kwa moja na mauaji dhidi ya Waislamu hao.
Ripoti mbalimbali za kuaminika zinaonyesha kuwa, baadhi ya Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakiuawa kwa kupigwa risasi na wanajeshi hao au kupitia hujuma ya mabudha wenye misimamo ya kufurutu ada ambao nao wamekuwa wakipata himaya ya jeshi.
Aidha Waislamu wa Rohingya wamekuwa wakipoteza maisha kwa kuzama boti wanazosafiria wakikimbia hujuma za mabudha na wengine hufa kwa njaa wakiwa njiani huku baadhi yao wakitangatanga katika misitu na baharini wakiwa katika juhudi za kukimbia vitendo vya utumiaji mabavu vinavyowalenga. 
Wanajeshi wa Myanmar wanaotuhumiwa kuwaua Waislamu wa Rohingya
Hii ni katika hali ambayo, baada ya kufanyika marekebisho ya kisiasa na kiuchumi nchini Myanmar walimwengu walikuwa wakitaraji kwamba, serikali ya nchi hiyo itachukua hatua ya kulipatia ufumbuzi tatizio la Waislamu wa Rohingya.
Kwani kimsingi hatua ya serikali ya Myanmar ya kuwanyima haki ya uraia Waislamu hao ndio iliyoandaa uwanja wa mauaji na vitendo vya kinyama dhidi yao.
Marie Lall, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Heidelberg  cha nchini Ujerumani na mtaalamu wa masuala ya Myanmar anasema: Baada ya kufanyika marekebisho ya kiuchumi na kisiasa nchini Myanmar, licha ya kuwa hali ya kifedha ya watu katika miji imeboreka, lakini faida ya hilo sio tu kwamba, na haiyafikii maeneo ya vijijini na viunga vyake, bali hali hii imezidisha mazingira magumu kwa akthari ya jamii za waliowachache kuweza kumiliki nyumba na makazi.
Mabudha wenye misimamo mikali wa Myanmar ambao wamekuwa wakiwahujumu na kuwaua Waislamu wa Kirohingya
Ramzy Baroud mwandishi wa habari Mmarekani mwenye asili ya Palestina ambaye anaishi Washington anasema: Baada ya Myanmar kuondolewa vikwazo, ulimwengu wa Magharibi ulipata fursa mwafaka ya kunufaika na vyanzo vya utajiri vya nchi hiyo na hili ni jambo ambalo linapewa kipaumbe na madola ya Magharibi kuliko hata suala la haki za binadamu. Ni kwa mintarafu hiyo ndio maana madola hayo yamenyamazia kimya mauaji dhidi ya Waislamu wa Myanmar na yanachokifuatilia katika nchi hiyo ni maslahi yao ya kiuchumi tu.
Vyovyote itakavyokuwa, inavyoonekana ni kuwa, nchi na asasi za Kiislamu ndizo zinazoweza kuchukua hatua za maana za kuhitimisha jinai za jeshi la Myanmar na mabudha wenye misimamo mikali dhidi ya Walislamu wa Rohingya. Indonesia na Malaysia zikiwa nchi za Kiislamu wanachama wa Jumuiya ya Nchi za Kusini na Mashariki mwa Asia ambapo Myanmar pia ni mwanachama katika jumuiya hiyo, zina jukumu zito zaidi la kuzuia unyama na ukatili dhidi ya Waislamu wa jamii ya Rohingya.
Huku utawala wa mabudha wa Myanmar ukiendeleza ukatili wake dhidi ya Waislamu wa Rohingya, utawala wa Kizayuni wa Israel unaowakandamiza kikatili Waislamu wa Palestina nao unaimarisha ushirikiano wake wa kijeshi na serikali ya Myanmar.
Gazeti la Haaretz la utawala wa Kizayuni limeripoti leo (Jumatatu) kuwa katika ziara ya mwaka jana ya nchini Myanmar ya Michel Ben-Baruch, mkuu wa kitengo cha utawala wa Kizayuni cha kusafirisha nje vifaa vya kijeshi, utawala wa Kizayuni ulikubaliana na nchi hiyo kuiuzia boti za kisasa za kivita.
Wahanga wakuu wa ukatili wa mabudha wa Myanmar wanaoungwa mkono na Israel ni watoto na wanawake Waislamu

Wakati huo huo afisa mmoja wa baraza la kijeshi la Myanmar mwaka 2015 alitembelea ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu na kuonana na mkuu wa jeshi wa Israel.
Kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa, Waislamu 90 elfu wamekimbia makazi yao katika jimbo la Rakhine katika kipindi cha siku 10 zilizopita kutokana na ukatili mkubwa wanaofanyiwa na wanajeshi wa serikali ya Kibudha ya Myanmar.
Serikali ya nchi hiyo inawanyima Waislamu karibu milioni moja wa Rohingya hata haki zao za kimsingi kabisa kama vile uraia. 
Hadi hivi sasa maelfu ya Waislamu wa Rohingya wameshauawa na makumi ya maelfu  ya wengine wamelazimika kuyakimbia makazi yao.

MWEZI WA MUHARRAAM NA UZUSHI

بسم الله الرحمن الرحيم MASHIA NA BIDAA ZA MWEZI WA MUHARRAMU. Mwezi wa Muharramu ni miongoni mwa miezi mitukufu kwa mujibu wa mafundis...