بسم الله الرحمن الرحيم
MASHIA NA BIDAA ZA MWEZI WA MUHARRAMU.
Mwezi wa Muharramu ni miongoni mwa miezi mitukufu kwa mujibu wa mafundisho ya kiislamu.
Mwezi huu tumefudishwa kufunga swaumu ya Ashuuraa na kufanya kheri nyinginezo kwa kutaraji malipo.
Mwezi huu una kumbukumbu kwa Waislamu kwa tukio kubwa la kuhama Mtume wa Allah Swalla llaahu alayhi wasalama kutoka Makkah kuhamia Madinah.
Allah mtukufu pia akajaalia kifo cha Husein lbnu Aliy Radhia llaahu anhu mjukuu wa Mtume swalla llaahu alayhi wasallama kutokea mwezi huu huko Karbala nchini lraqi kwa kuuwawa kwa dhulma.
Mashia wakachukua tukio la kifo cha Husein Radhia llaahu anhu ndani ya mwezi huu kufanya maadhimisho yaliyo jaa Bidaa na Munkari na kuziacha Sunna zenye fadhila ndani yake, wakajibidisha kutekeleza Bidaa wanazo amini ni kukienzi kizazi cha Mtume Swalla llaahu alayhi waalihi wasallama.
Mashia weameacha Sunna ya kufunga mwezi huu (Ashuuraa) huku wakiwatuhumu wote wanaofunga wanafunga kwa kuunga mkono na kusherehekea kuuwawa Husein lbnu Aliy Radhia llaahu anhu.
Mashia wapo baadhi yao hawali nyama mwezi huu wa Muharram hususan siku ya mwezi kumi,siku ambayo ameuliwa Husein lbnu Aliy Radhia llahu anhu,kwa kudai siyo vizuri siku ambayo damu ya mjukuu wa Mtume swalla llaahu alayhi wasallama imemwagika halafu wao wale nyama.
Wakristo nao baadhi yao hawali nyama siku ya ljumaa kuu ya Pasaka,siku ambayo wanadai Yesu aliteswa na kuuwawa Msalabani,hivyo haiwezekani kula nyama siku ambayo kiongozi wao amemwaga damu Msalabani.
Wapo Mashia ambao hawawezi kufunga ndoa mwezi huu kwa kudai ndoa ni jambo lenye furaha ,nao wako ndani ya huzuni hawawezi kufanya jambo la furaha, ni sawa na kupuuza kifo cha Husein Ibnu Aliy.
Mwezi huu ni mwezi wa kuimba nyimbo za kuomboleza msiba na kulaani waliomuua Husein na wengine wote wanaopinga maadhimisho yao huku wakiwatuhumu kufurahia au kutojali mauaji hayo.
lmekuja katika kitabu مفاتيح الجنان mlango unaozungumzia matendo ya mwezi wa Muharram.
وينبغي للشيعة أن يمسكوا عن السعي في الحوائج دنياهم وأن لايدخروا فيه شيأ لمنازلهم وأن يتفرغوا فيه للبكاء والنياح وذكر المصائب،وأن يقيموا مآتم الحسين عليه السلام، وأن يجتهدوافي سب قاتليه ولعنهم ،والأ حسن لايصام اليوم التا سع والعاشر فإن بني أمية كانت تصومها شماتة بالحسين عليه السلام وتبركا بقتله،وقد افترواعلى رسول الله صلى الله عليه وآله وسلم أحاديث كثيرة وضعوها في فضل هاذين يومين وفضل صيامهما( مفاتيح الجنان،فصل في أعمال شهر محرم،ص352-353،دار القربى للطباعة والنشر)
lnatakiwa Mashia wajizuilie kutembea kwa ajili ya mambo ya dunia yao siku hiyo ya Ashura,na wasilimbikize chochote majumbani mwao,na wakae faragha kwa ajili ya kulia na kuomboleza na kutaja matukio (kuhusu Husein) na wajipige kifuani kwa ajili ya Husein amani juu yake,pia wajitahidi kuwatukana waliomuua na kuwalaani,na wapeane pole wenyewe kwa wenyewe(Taazia).Na lililo bora wasifunge siku ya tisa na kumi (Mwezi Muharram) hakika banu Umayyah walikua wanafunga masiku hayo kufurahia kifo cha Husein alayhi ssalaam na kutaka baraka kwa kifo chake.Hakika (hao banu Umayyah)wamezusha hadithi nyingi juu ya Mtume swalla llaahu alayhi wasallama wakaweka katika fadhila za masiku haya mawili (9 - 10) na fadhila ya swaumu yake.
(Mafaatiyhul Jinaan,mlango,Matendo ya mwezi wa Muharramu,Uk 352-353,chapa ya Daarul Qurbaa).
Je Mashia wanafunga mwezi Muharram kama wafungavyo Waislamu wengine?.
وينبغي أيضا للشيعة الإمساك عن الطعام والشراب في هاذا اليوم من دون نية الصيام وأن يفطروا في آخر النهار بعد العصر بما يقتات به أهل المصا ئب كاللبن الخا ثر والحليب. ونظا ئر هما لا با لأغذية اللذيذة.
Na yatakikana pia kwa Mashia kujizuilia kula na kunywa siku hii pasi na kunuia kufunga na wafuturu mwishoni mwa mchana baada ya Al asri kwa kile walichokula watu wa masaibu (ya Karbala) kama maziwa na maziwa ya mgando na muonekano wake isiwe chakula kitamu.(Rejea ni hiyo hiyo hapo juu).
Wakristo nao hufunga msimu wa Pasaka siku 40 mfululizo,kuanzia mwezi wa tatu wote (March)hadi masiku kumi ya mwanzo ya mwezi wa nne (April),mwezi wa nne ndiyo mwezi wa Pasaka, hujizuia kula na kunywa ,funga hii wanafungua sa 12 jioni ,na wenye matatizo kama maradhi wanaweza kufungua saa 9 au 10, lengo la kufunga ni kushinda na njaa kama alivyo shindaYesu kwa siku arobaini.Mashia nao wanashinda na njaa hadi jioni (Al asri) kama walivyo shinda watu wa tukio la mauaji ya Husein Karbalaa.
Ukimuuliza Shia juu ya Bidaa wazifanyazo mwezi wa Muharramu uhalali wake katika dini atakushutumu hukipendi kizazi cha Mtume swalla llaahu alayhi wasallama,au utaishia kuambiwa wewe ni Wahabi tu,una chuki na Ahlul Bayti,au umebahatika utajibiwa hayo yanayo fanywa ya kujipiga kijitoa damu,kutembea juu ya moto ,kubeba majeneza na mikuki huo ni ujinga wao tu hao wafanyao,kwani hayamo katika Ushia.
Ni kweli hayamo katika Ushia? Wenyewe watatufahamisha kupitia vitabu vyao.
(a)KUCHANA NGUO KWA AJILI. YA MSIBA.
عن حيان بن سديرقال،سألت أبا عبد الله عليه السلام عن الرجل شق ثوبه على أخيه أو على أخته أو على قريب له؟فقال لابأس بشق الجيوب فقد شق موسى بن عمران عليه السلام جيبه على أخيه هارون(تهذيب الإحكام،8/325،وسائل الشيعة22/304)
Amesimulia Hayyaan lbnu Sadiyr(au Sudayr) amesema,Nilimuuliza Abu Abdillaahi alayhi ssalaam juu ya mtu aliye chana nguo juu msiba wa nduguye,au dada yake,au mtu wa karibu yake?akasema hapana shaka (kwa ajili ya msiba)ni sawa kuchana nguo. Hakika amechana Musa lbnu lmraan nguo yake juu ya kifo cha nduguye Haarun.(Tahdhiybul Ahkaam 8/325,Wasaailu Shiiah 22/304).
(b)KUJIPIGA MAKOFI.
Amesema mwandishi wa kitabu Ashaairul Husayniyah,Sheikh Muhamad Jumaa Baadiy.
ومن حق هؤلاء الذين لم يعرفوا الحسين عليه السلام ولم يشربوا كأس محبته ولم يحزنوا في مصيبته أن يتعجبوا من مظا هر الشيعة في أحزانهم عليه ،فإن حبهم المتجذر في النفوس دفعهم إلى لطم الصدور ووجوه والرؤوس في المآتم.(الشعائر الحسينية،ص134، اللطم).
Kutokana na ukweli wa hawa ambao hawamjui Husein alayhi ssalaam,na hawaja kunywa kikombe cha mapenzi yake,na hawahuzuniki kwa msiba wake wanastaajabia muonekano wa Mashia katika kumuhuzunkia huyo (Husein) Hakika mapenzi yao ni yenye kuchipua kutoka nafsini mwao,yakawasukuma kupiga vifua na nyuso na vichwa katika maombolezo.(Ashaairul Husayniyyah Ukr 134).
Wanasema Mashia hata Malaika (Mahurlul ayni) Peponi hujipiga makofi kwa ajili ya Husein,kwa maana inayopatikana katika ziara ya Swaahibul Aswri alayhi ssalaam (Imam Mahdi),pale alipo mzuru babu yake Husein alayhi ssalaam alisema.
"وأقيمت لك المأتم في أعلى عليين،ولطمت عليك حور العين"(بحار الأنوار 97/322).
Na wamefanya(Malaika) maombolezo kwa ajili yako juu mbingu ya saba,Na wamejipiga makofi kwa ajili yako(Mahuuril ayni) Malaika wa peponi.(Bihaarul Anwaar 97/322)
(c)KUJIKATA MIILI YAO HADI KUTOA DAMU.
Amesema mwandishi Mshia wa kitabu Ashaairul Husayniyyah ukurasa wa 138.
وظاهر فتاوى كثير من العلماء الإعتماد على هذا الخبر المرسل في جواز الإدماء،وأفتى عامة الفقهاء برجحا نه واستحبابه لكونه أجلى مصاديق الجزع علئ الإمام الحسين عليه السلام عملا بهذه الرواية.
Na dhahiri fatawa za wengi miongoni mwa Maulamaa ni (kwamba).wanaitegemea habari hii ambayo ni mursal (juu ya kujipiga na) kujitoa damu,na wanachuoni wote wa fiqhi wametoa fatwa kwa kulipa nguvu (hilo) na kulipendekeza kwa kuwa ni jambo kubwa zaidi lenye kujulisha kumuhuzunikia Husein alayhi ssalaam kwa ajili ya kuifanyia kazi riwaya hii.
Anachosema ni kwamba wanachuoni wa kishia wameitegemea riwaya Mursal (Hadithi dhaifu) kutoa fatwa kujuzisha kujipiga na kujitoa damu,ila huko kujipiga na kujitoa damu wanafanya kwa sababu kunaonyesha kumuhuzunikia lmam Husein.
Akaeleza tena juu ya hilohilo la kujitoa damu.
قال الشيخ محمد حسين النا ئيني ،لاإشكال في جواز اللطم بالأيدي على الخدود والصدور إلى حد الإحمرار والإسوداد،بل يقوى جواز الضرب با لسلاسل أيضا على الأكتاف والظهور إلى حد المذكور ،بل وإن تأدى كل من اللطم والضرب إلى خروج دم يسير على الأقوى،وأما إخراج الدم من النا صية با لسيوف والقامات فالأقوا جواز ما كان ضرره مأمونا ،وكان من مجرد إخراج الدم من النا صية بلا صدمةعلى عظمها،ولا يتعقب عادة بخروج ما يضر خروجه من الدم ونحوذلك كما يعرفه المتدبرون العارفون بكيفية الضرب ولوكان عند الضرب مأمون ضرره بحسب العادة،ولكن إتفق خروج قدر ما يضر خروجه لم يكن ذلك موجبالحرمته،ويكون كمن توضأ أو اغتسل أو صام أمنا من ضرره ثم تبين ضرره منه (الشعائر الحسينية ص 144،وفتاوى الشعائر الحسينية،ص21)
Amesema Sheikh Muhamad Husein Annaaiyniy,Hakuna shaka juu ya kufaa kujipiga kwa mikono mashavuni na kifuani mpaka kujitia wekendu na weusi,bali inapata nguvu kauli ya kufaa kujipiga kwa minyororo juu ya mabega na mgongoni mpaka kufikia hivyo ilivyo tajwa(wekundu na weusi),Bali hakuna ubaya hata kama itapelekea kutoka damu kidogo kwa kauli yenye nguvu,Ama kujitoa damu utosini kwa Upanga na ncha zake,kwa kauli yenye nguvu inajuzu kiasi cha kuwa madhara yake siyo makubwa kwa kiasi cha kujitoa damu kwenye utosi pasi na kuugonga mfupa wake na isifuate kutoka kile ambacho kina madhara(iwe ubongo) ,kama wanavyo jua hilo wenye wenye uzoefu kuhusu namna ya kujipiga na hata kama wakati wa kujipiga anakua ni mwenye kujiaminisha na madhara,LAKINI AKITOA DAMU KIASI CHENYE KUJIDHURU BASI HILO SIYO HARAMU,ni sawa na mtu aliye tawadha ,kuoga au kufunga akiwa na amani kwamba hatodhurika kisha akapata madhara.(Ashaairul Husayniyah Ukr 144,Fataawa,Shaairul Husayniyah Ukr 21).
Kama kawaida ya Mashia,jambo lao hawakosi kulijaza fadhila nyingi ili liendelee kudumishwa hata kama liko kinyume kabisa na mafundisho ya Uislamu,zifuatazo ni Riwaya zao juu ya fadhila za kuzuru kaburi la Husein Radhia llahu anhu huko Karbalaa nchini lraqi.
عن بشير الدهان قال،سمعت أبا عبد الله عليه السلام ،من زارقبر الحسين عليه السلام يوم عرفة،فكأنما زار الله تبارك وتعالى في عرشه. (بحار الأنوار 87/97)
Amesimulia Bashir Adahhaan amesema,Nimemsikia Abuu Abdillaahi alayhi ssalaam,Mwenye kuzuru kaburi la Husein alayhi ssalaam siku ya Arafa,kana kwamba amemzuru Allah mtukufu katika Arshi yake.(Bihaarul Anwaar 87/89)
عن داود بن كثير،عن أبي عبد الله عليه السلام قال، إن فاطمة بنت محمد عليها السلام تحضرلزواز قبر ابنها الحسين عليه السلام فتستغفر لهم ذنوبهم(كامل الزيارات)
Amesimulia Daud lbnu Kathir,kutoka kwa Abuu Kaa alayhi ssalaam amesema, Hakika Fatma bint Muhammad alayha ssalaam,anahudhuria kwa wanaolizuru kaburi la mtoto wake Husein amani juu yake na anwaombea msamaha madhambi yao.(Kaamilu Ziyaaraati)
عن إسحاق بن عمار قال،سمعت أبا عبد الله عليه السلام يقول،ليس النبي في السماوات والأرض إلا يسألون الله تعالى أن يأذن لهم في زيارة الحسين عليه السلام،ففوج ينزل وفوج يصعد(كامل الزيارات-البحار101)
Amesimulia Ishaqa lbnu Ammar amesema,Nimemsikia baba Abdillahi alayhi ssalaam anasema,Hakuna Nabii mbinguni na ardhini ila anamuomba Allah mtukufu amruhusu (ahudhurie) katika kumzuru Husein alayhi ssalaam,makundi wanateremka na makundi wanapanda.(Kaamilu Ziyaaraati -Albihaaru 101)
عن يونس،عن أبي عبد الله عليه السلام قال،من زار قبر الحسين عليه السلام يوم عرفة،كتب الله أالفاألفا حجة مع القائم،وإلفا ألفا عمرة مع رسول الله صلى الله عليه وسلم(كامل الزيارات ص172)
Amesimulia Yunus,kutoka kwa Abuu Abdillahi alayhi ssalaam amesema,Mwenye kuzuru kaburi la Husein alayhi ssalaam siku ya Arafa,humuandikia Allah maelfu kwa maelfu ya hija pamoja na lmam Mahdi,na maelfu kwa maelfu ya Umra pamoja na Mtume swalla llaahu alayhi wasallama(Kaamilu Ziyaaraati,Ikr 172)
عن أبي عبد الله عليه السلام قال،طين قبر الحسين الشفاء من كل داء وهو الدواء الأكبر(البحار 101)
Amesimulia Abu Abdillahi alayhi ssalaam amesema,Udongo wa kaburi la Husein ni dawa ya kila ugonjwa,nao ni dawa kubwa(Albihaaru 101)
قال الصادق عليه السلام،السجود على طين الحسين ينور إلى أرض السابعة(الفقيه ج-1)
Amesema Aswaadiqu alayhi ssalaam,Kusujudu juu ya udongo wa (Kaburi la Husein) kunatoa nuru mpaka ardhi ya saba (Alfaqiyhu- jz-1)
عن أبي عبد الله عليه السلام قال، من أتى الحسين عارفا بحقه كتب الله في أعلى عليين(البحار 101)
Amesimulia Abuu Abdillahi alayhi ssalaam amesema,Mwenye kumuendea Husein huku akijua haki yake humuandika Allah juu mbingu ya saba(Albihaaru 101)
عن علي بن أسبط ،عن أبي عبد الله علبه السلام ،قا ل إن زيارة قبر الحسين عليه السلام أفضل من حج بيت الله الحرام،بل إن زوار الحسين أطهار،وأهل الموقف فيهم إبناء زنا(بحار الأنوار 87/98)
Amesimulia Aliy lbnu Asbaatwi, kutoka kwa Abuu Abillaahi alayhi ssalaam amesema,Hakika kuzuru kaburi la Husein alayhi ssalaam ni bora kuliko kuhiji nyumba ya Allah tukufu (Alkaaba) Lakini hakika wanaomzuru Husein wametwaharika,na watu wa Arafa katika wao kuna watoto wa Zinaa(Bihaarul Anwaaru 87/98)
عن أبي عبد الله عليه السلام قال،إن الله تبارك وتعالى ليبدأ بأهل قبر الحسين عليه السلام قبل أهل العرفات(بحار الأنوار 87/98)
.
Amesimulia Abuu Abdillahi alayhi ssalaam amesema,Hakika Allah mtukufu huanza (kuwatazama) watu waliopo kaburi la Husein alayhi ssalaam,kabla ya watu waliopo Arafah (Bihaarul Anwaar 87/98).
Kwa mujibu wa fadhila hizi za kuzuru kaburi la Husein Radhia llaahu anhu huko Karbala lraqi basi Mashia kwao Hija haina thamani mbele ya kuzuru kaburi la Husein Radhia llaahu anhu.
Jambo la Husein limeleta mtihani kwa Mashia kama ifuatavyo.
(1)Wapo wanao huzunika tu,
(2)Wengine hudondosha machozi.
(3)Wengine hulia kwa kwikwi.
(4)Wengine hupiga mayowe.
(5)Wapo wanaojipiga kifuani.
(6)Wengine hujipiga makofi.
(7)Wengine hujipiga utosini.
(8)Wengine huchana nguo zao.
(9)Wengine hujipiga minyororo mabegani.
(10)Wengine hujipiga visu migongoni.
(11)Wengine hijikata upanga utosini au mgongoni.
(12)Wengine huchomwa sindano utosini na kutolewa damu.
(13) Wengine hubeba majeneza na mikuki.
(14)Wapo wanao jitaabisha kwa kuswali au kutembea juu ya moto.
(15)Wapo wanao tambaa kwa tumbo kuliendea kaburi la Husein huko Karbalaa
(16)Wapo wanao muadhibu mnyama kwa niaba ya mtu ambae wanaamini alikua ni adui wa Ahlul Bayti kama Yazidi lbnu Muawiyah na wengineo wanao watuhumu ubaya dhidi ya Ahlul Bayti.
Yote haya hufanyika kwa madai ya kumpenda Husein na huzuni juu yake,ukipinga unahukumiwa kuwachukia Ahlul Bayti.
La kushangaza,wameuliwa Manabii alayhimu Ssalaam kwa dhulma lakini wafuasi wao hawakufanya haya,wameuliwa Maswahaba kama Hamza na wengine Allah awaridhie,lakini Mtume swalla llaahu alayhi wasallama hakufanya haya wafanyayo Mashia.
Amekufa Mtume swalla llaahu alayhi wasallama, na Mashia wanasema ameuliwa na wake zake wawili Aisha na Hafsa Allah awaridhie kwa kumnywesha Sumu nacho ni kifo cha dhulma, Mtume pia alikuwa mtetezi wa haki kwa Ulimwengu wote,mbona Ahlul Bayti hawakufanya hayo?,na mbona Mashia hawaombolezi kifo cha Mtume kwa vishindo nao wanadai ameuliwa kwa dhulma?,Au Mtume hakua mtetezi wa haki za watu wote kama Husein?.
(Kuuhusu Mtume kuuliwa na wake zake,Tazama tafsiri ya Mayunga chapa ya pili ukrasa wa 187 na Alburhan fiy tafsiri lqur-an ya Sayyid Haashimul Bahraaniy katika ufafanuzi wa Surati Ttahriym aya ya 1 -2. kifungu cha 5,hao wote ni Mashia).
Mashia mila hii wameitoa wapi?
Mila hii ya kutomaliza kuomboleza msiba waanzilishi ni Wakristo,kama waombolezavyo kifo cha nabii lsa alayhi ssalaam kila mwaka kwa vilio ,matembezi na kujipiga au kumtungika mmoja wao Msalabani wakamsulubu pengine hadi kifo hasa sehemu za Amerka ya kusini.Mashia nao husimama Sayyid wao na upanga mkononi akiwachanja utosini wafuasi wake wakiwemo na watoto wadogo wasiojua maaa ya jambo hilo,nako ni kuwasulubu pia hakika mwili hauchezewi kiurahisi sampuli hiyo.
Mashia wa huku kwetu kuna mambo hawajafikia kuyafanya kwa sababu imani zao hazijakomaa kama Mashia wa huko Asia,wasitudanganye kwamba hayamo katika Ushia ,ukweli yameruhusiwa tena ni kiwango cha juu cha mapenzi ya Husein Radhia llaahu anhu.
TANBIHI.
Waliofia Karbala wameuliwa hawakujiua,wewe ukijiua kwa kujipiga au kujitoa damu umejiua mwenyewe,Amesema Allah mtukufu.
قُلْ هَلْ نُنَبِّئُكُمْ بِالْأَخْسَرِينَ أَعْمَالًا
Sema: Je, tukutajieni wenye khasara mno katika vitendo vyao?(Alkahfi 103)
الَّذِينَ ضَلَّ سَعْيُهُمْ فِي الْحَيَاةِ الدُّنْيَا وَهُمْ يَحْسَبُونَ أَنَّهُمْ يُحْسِنُونَ صُنْعًا
Ni wale ambao juhudi yao katika maisha ya dunia imepotea bure, nao wanadhani kwamba wanafanya kazi nzuri.(Alkahfi 104)
Tunamuomba Allah atuonyeshe haki na tuweze kuifuata.
والله أعلم.